Jeshi
ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa wito kwa madereva
bodaboda katika Jijini la Dar es salaam, kuacha kufanya shughuli hiyo
ifikapo majira ya saa 6 usiku ili kupunguza uhalifu.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema
kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia mwanya katika muda huo
kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha pikipiki.
Aidha,
Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18 hadi 23 Jeshi la Polisi
Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460
kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki
1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika
njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.
Kuhusu
suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana
kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na
kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247
kutokana na oparesheni inayoendelea.
Alisema
baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa mahakamani kwani upelelezi bado
haujakamilika na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
0 comments :
Post a Comment