Mwanafunzi wa kwanza katika matokeo ya kidato cha nne nchini kutoka shule ya Sekondari ya Feza Boys jijini Dar es Salaam, Alfred H. Shauri (katikati) akielelzea siri ya mafanikio yake kwa wanahabari. |
MWANAFUNZI wa kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
mwaka 2016, Alfred H. Shauri, ameeleza siri ya mafaniko yake kuwa
ilitokana na kusoma kwa bidii na kumtanguliza Mungu katika kila
alichofanya.
Akizungumza na wanahabari katika Shule ya Sekondari ya Feza Boys
alikosoma eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam, amesema kitu cha
kwanza katika kila alilofanya ni kumtanguliza Mungu katika masomo yake
na cha pili alikuwa sambamba na wazazi wake kuhakikisha anachukua
ushauri wao juu ya masomo yake ambapo kwa uapnde wa walimu wake alisema
aliwasikilza kwa makini na kuwauliza maswali pale alipokuwa akihitaji
msaada na kujisomea vitabu mbalimbali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Sekondari za Feza, Ibrahim Yunus,
alisema kuwa mafaniko ya mwanafunzi huyo yametokana na juhudi zake
mwenyewe alizokuwa nazo wakati akiwa shuleni hapo kwani aliweza kuwa wa
kwanza pia katika shindano la insha iliyozikutanisha shule za Afrika
Mashariki mwezi Mei mwaka jana.
0 comments :
Post a Comment