Majanga Yaendelea Kumwandama Yusuf Manji.......Duuuh!


Idara  ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imesema inakusudia kumfungulia mashtaka mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji kwa kosa la kuajiri wafanyakazi wageni 25 wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini kupitia Kampuni ya Quality Group.

Wakati Uhamiaji wakisema hivyo, Julai 15 mwaka jana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari , akieleza kuwa amestaafu rasmi nafasi hiyo.

Katika taarifa hiyo Manji alisema baada ya kustaafu atabakia kuwa mshauri huku akitaja  sababu za kufanya hivyo kuwa ni utaratibu uliokuwa umewekwa na waasisi wa kampuni hiyo wa kuwa na ukomo wa uongozi usiozidi miaka 20.

Katika taarifa hiyo alieleza kuwa ameshatumikia nafasi hiyo kwa miaka mingi na ni muhimu kutoa fursa kwa kiongozi mwingine ili aweze kujishughulisha na shughuli nyingine ikiwamo kufundisha katika vyuo vikuu ujasiriamali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna wa Idara hiyo, John Msumule alisema kazi hiyo itafanyika baada ya mfanyabiashara huyo kutoka hospitali alikolazwa akiendelea na matibabu ambapo ataunganishwa  na kesi hiyo na lazima afikishwe mahakamani.

“Jumla ya wafanyakazi walikuwa 128, kati yao wawili walikimbia nchi na kubaki 126 na baada ya ukaguzi tuliwabaini wengine 25 wakiwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini.

“Taratibu zetu ni kuwafungulia mashtaka waliokamatwa lakini pia tutamfikisha mahakamani muajiri wao kwa kufanya makosa hayo huku akijua ni kinyume na sheria,” alisema Musumule.

Alisema walianza kufanya ukaguzi katika kampuni hiyo  Ijumaa ya wiki iliyopita lakini hawakupewa ushirikiano ambapo walimkamata msaidizi wake.

“Siku ya Jumamosi walikuwa na passport hapa lakini wafanyakazi wawili walikimbia nchi na ndipo tulipogundua kuna 25 wanaofanya kazi katika kampuni hiyo bila kuwa na kibali,”alisema Musumule.

Mbali na hilo alisema wamefanikiwa kumkamata raia wa Uganda, Asha Talib ambaye alikuwa na makosa ya kuishi nchini bila kibali, kuhondhi hati za kusafiria 15 za raia wa Uganda na tatu za Madagaska.

Mtuhumiwa huyo alipokuwa akihojiwa mbele ya waandishi wa habari alidai kuwa alikuwa anafanyakazi katika kampuni inayoshughulika na maombi ya viza kwa njia ya mtandao ambapo bosi wake raia wa Tanzania alikimbia.

“Kazi tuliyokuwa tunafanya ni kuwapatia watu mbalimbali viza baada ya kufanya maombi kwa njia ya mtandao na kisha kuwatumia viza hizo za kusafiria huko waliko,” alisema Talib.

Aidha katika hatua nyingine Kamishna Musumule alisema kuwa kuna baadhi ya watumishi wa idara hiyo wasiokuwa  waminifu ambao wamekuwa wakishiriki katika kughushi hati mbalimbali za kusafiria.

“Wiki ijayo nendeni Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji ambapo tutawatangazia hatua ambazo tumezichukua juu ya watumishi hao ambao si waaminifu,”alisema Musumule.

Alisema katika operesheni hiyo,  walikamata vibali bandia nane vya raia wa China wa Kampuni ya Global Leader na ukaguzi uliofanyika katika jengo la Diamond Plaza walibaini Kampuni ya Luck Spin.

“Pia tumefanikiwa kumkamata mwajiri raia wa Tanzania kwa kumwajiri mgeni kutoka nchini Malawi katika kampuni ya ulizi kinyume cha sheria,” alisema Musumule.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment