Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Ilala, Salum Hamdani wamechuana mahakamani katika kesi ya uchochezi
inayomkabili mbunge huyo na wahariri wa gazeti la Mawio.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba leo atatoa uamuzi wa kama
Hamdani aeleze anachokifahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha
anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
Hiyo ilikuwa ni baada ya Lissu kumtaka Hamdani, ambaye ni shahidi wa
upande wa mashtaka, aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar na
kama Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
Hakimu Simba alifikia uamuzi huo baada ya wakili wa Serikali, Paul
Kadushi kupinga shahidi huyo kujibu swali hilo kwa sababu si mtaalamu wa
sheria wala katiba hivyo hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na
kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza
masuala ya kikatiba.
Lissu alimhoji Hamdani maelezo yake yaliyo polisi aliyaandika kama nani? Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Hamdani: Niliandika maelezo yangu kama mlalamikaji na kwamba mikusanyiko hiyo haikuwa haramu, ilikuwa halali kisheria.
Lissu: Mweleze mheshimiwa kama mihemko kisheria inakatazwa ama la?
Hamdani: Haikatazwi.
0 comments :
Post a Comment