Mabingwa wa nchini Ufaransa timu
ya PSG imefanya maafa baada ya kuitwanga Barcelona kwa mabao 4-0 katika
mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya.
Barcelona ikiwa ugenini jijini
Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake
Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo
mchovu.
Angelo Di Maria ametumbukia
nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga
moja na Julian Draxler akifunga moja.
Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0.
Michuano hiyo itaendelea tena leo
kwa Michezo miwili Bayern Munich watawaalika Arsenal huku Mabingwa
watetezi wa Kombe hilo Real Madrid watacheza na Napoli toka Italia
0 comments :
Post a Comment