Raundi ya Sita ya mechi za kuwania
Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup –
2016/17, itaanza Februari 16, 2017 badalay a Februari 24, mwaka huu.
Mchezo huo awali ulipangwa
kufanyika Machi mosi, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja kabla ya kuendelea
tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo
kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00
jioni.
Michezo hiyo kwa mujibu wa
ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu yaP wani watakaocheza
kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar
itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati
ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam naMtibwa Sugar
watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, mwaka
huu timu yaM bao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City
zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenyeUwanja waTaifa jijini Dar Es Salaam.
0 comments :
Post a Comment