Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ameyataka majeshi yote hapa nchini yajipange kuendana na sera ya ujenzi
wa viwanda kwa kuhakikisha viwanda vya kutengeneza mahitaji yanayoweza
kupatikana hapa nchini
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo leo mara baada ya kumuapisha Jenerali
Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania katika
hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Ametoa
wito kwa uongozi mpya wa Jeshi hilo chini ya Jenerali Venance Mabeyo
kuendeleza juhudi za kuilinda nchi na kuhakikisha viwanda vya kuzalisha
bidhaa mbalimbali kwa ajili ya majeshi kama vile sare na vifaa,
vinajengwa.
Rais
Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Davis
Mwamunyange kwa kuliongoza jeshi hilo kwa kipindi chote alichokuwa
madarakani na kueleza kuwa watanzania wana imani kubwa na JWTZ.
Kabla
ya kuapishwa kushika wadhifa wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Rais
Magufuli amemvalisha Jenerali Venance Salvatory Mabeyo cheo kipya cha
Jenerali alichopandishwa kutoka Luteni Jenerali.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa
kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Luteni
Jenerali James Alois Mwakibolwa amechukua nafasi iliyoachwa wazi na
Jenerali Venance Salvatory Mabeyo ambaye sasa ni Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Kamishna Juma Ali Malewa kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kabla ya kuapishwa kushika wadhifa huo, Mhe. Rais Magufuli amevalisha Kamishna Juma Ali Malewa cheo kipya cha Kamishna Jenerali.
Kamishna Jenerali Juma Ali Malewa amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna John Casmir Minja ambaye amestaafu.
Halikadhalika,
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Balozi. Luteni Jenerali Mstaafu
Paul Meela kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Mhe. Balozi Luteni Jenerali Mstaafu Paul Meela anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Antony Ngereza Cheche ambaye amestaafu.
Pia, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Balozi Samuel Shelukindo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
Mhe. Balozi Samuel Shelukindo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Balozi Begum Taj ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Bw. Nyakimura Mathias Muhoji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Bw. Nyakimura Mathias Muhoji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Claudia Mpangala ambaye amestaafu.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia tukio la kuapishwa kwa
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Robert Boazi
Mikomangwa.
Kamishna Robert Boaz Mikomangwa ameapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali wa Polisi - Ernest Mangu.
hafla
hiyo imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,
Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma na Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli.
==> Msikilize Hapo Chini Akiongea.......



0 comments :
Post a Comment