Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wapya watatu ambao aliwateua tarehe
03 Desemba 2016.
Mabalozi
hao waliopangiwa vituo ni Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania
nchini Ubelgiji, Omar Yussuf Mzee anayekuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania
nchini Algeria na Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa
wazi na Dkt. Ladis Komba nchini Uganda ambaye amestaafu kwa mujibu wa
Sheria.
Aidha,
Balozi Sokoine ambaye anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na
Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Balozi
Mzee kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alishawahi kushika nafasi
mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nafasi ya mwisho alikuwa Waziri wa
Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya kwanza ya Rais
Dkt. Ali Mohammed Shein.
Kwa upande wa Balozi Mgavano kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ubalozi alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
Mabalozi
wote waliopangiwa vituo vya kazi wataapishwa na Rais Ikulu jijini Dar
Es Salaam leo Jumapili tarehe 12 Februari 2017 saa tano asubuhi.
0 comments :
Post a Comment