Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad
Masauni ametolea ufafanuzi kuhusu hatua inayochukuliwa na vyombo vya
dola dhidi ya watu wanaohusika na vitendo vya unyanyasaji vikiwemo
kupiga watu.
Naibu waziri huyo ametoa ufafanuzi huo
Jumatano hii mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati
alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.
Mbilinyi aliuliza, “Kumekuwa na tabia za
watu kupiga watu wengine, vipigo ambavyo vinafikia kiasi cha utesaji
matukio kama yaliyotokea Mbeya Day sekondari kwa mwalimu kumshambulia
mwanafunzi lakini na lile la mtu kumtoa macho mwingine tukio lililotokea
kule Buguruni, Je, Serikali inachukua hatua gani kwa watu wanaowapiga
wenzao bila sababu?”
Mheshimiwa Masauni alijibu, “Ni kweli
hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya kusikitisha katika nchi yetu na
kwa jamii ambavyo ni kinyume na sheria na havikubaliki. Aidha serikali
haikubaliani na vitendo vya namna hiyo vinavyofanywa na watu, mtu au
kikundi kwani vitendo hivyo ni kinyume na sheria na utaratibu mzima wa
haki za binadamu. Serikali kupitia jeshi la polisi imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali ili kuzuia na kulinda raia na mali zao, aidha serikali
kupitia jeshi la polisi tumepokea taarifa za matukio mbalimbali na
kuyafanyia uchunguzi wa kina yanapobainika upo ushahidi wa kutosha
mtuhumiwa huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria.”
Aliendelea, “Nichukue fursa hii kuwaasa
wale wote wanaokiuka taratibu, kanuni na sheria za nchi waache tabia
hiyo mara moja wizara yangu haitakuwa na suluhu kwa mtu yeyote
atakayetenda uhalifu huo.”
Ameongeza “Kuhusiana na suala la walimu
ambao wamewanyanyasa wanafunzi kwenye shule ya Mbeya day, suala hili ni
suala mtambuka kwahiyo ni hatua mbalimbali zinachukuliwa na mamlaka
husika kwa upande wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na mkurugenzi wa
mashtaka ni kwamba kuna hatua zinaendelea kuchukuliwa na pale ambapo
uchunguzi utakamilika watafikishwa katika vyombo vya sheria.”
0 comments :
Post a Comment