Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dar es Salaam .(Picha na Lorietha
Laurence-WHUSM).
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea na wadau wa michezo katika
ufunguzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
ulioanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi akisoma risala wakati wa ufunguzi
wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulioanzishwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu lengo ikiwa ni kubuni vyanzo mbalimbali vya
rasilimali ili kuwezesha shirikisho hilo katika kutekeleza kazi zake.
Mkuu wa Kitengo cha Ufundi wa
Maendeleo ya Soka nchini Bw. Kim Poulsen akiongea na wadau wa michezo
katika uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi katika
hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
leo Jijini .
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kushoto ni Meneja wa PPF Kanda ya
Ziwa Meshack Bandawe, Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel
Beatrice Singano na kulia ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NBC Salmi
Rupia.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi nyaraka za Bodi ya
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kwa Meneja wa PPF Kanda ya
Ziwa Meshack Bandawe (kushoto), ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo ,katikati
ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal
Malinzi.Leo Jijini dar es Salaam.
……………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imeunga mkono
uwanzishwaji wa Bodi ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu (TDF) wenye lengo
la kuratibu vyanzo mbalimbali vya mapato ili kutekeleza maendeleo ya
mpira nchini ikiwemo kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wa kike na wa
kiume.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipozindua
Bodi hiyo iliyo chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wadau wa
michezo,wananchi na sekta binafsi kuunga mkono jitihada hizo.
“Jambo hili ni jema sana katika
sekta ya michezo nchini hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaunga
mkono juhudi hizi zenye lengo la kuleta matokeo chanya katika sekta hii
muhimu mfano mzuri ni vijana wetu wa Serengeti Boys wameshatuonyesha
kuwa tunaweza kufika mbali” alisema Waziri Nnauye.
Aidha, aliitaka Bodi hiyo kufanya
kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuhakikisha mfuko huu unakua na hivyo
kuwezesha utendaji fanisi wa kukuza vipaji vya michezo wa kike na wa
kiume na kwa wale watakaokiuka miiko ya kazi uongozi usisite kuchukua
hatua za kinidhamu dhidi yao.
Naye, Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu wa Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi alieleza kuwa lengo la
kuunda mfuko huo ni kusaidi katika kuendesha shughuli za Shirikisho
ambapo kutakuwa na utaratibu maalum wa kuomba fedha kutoka katika mfuko
huo.
“Kiutaratibu Sekretrarieti ya TFF
ikiwa na mahitaji itakuwa inatuma maombi kwenda bodi na pale bodi
inaporijiridhisha na uhalali wa maombi hayo itatoa ruhusa kwa Shirikisho
kuendelea na utaratibu wa kupatiwa fedha “alisema Bw.Malinzi.
Bw. Malinzi aliongeza kwa kuahidi
kuwa TFF itahakikisha Tanzania inang’ara kimataifa katika mpira wa
miguu kwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2026 kwa upande
wa wanaume (Taifa Stars) na kwa upande wa wanawake (Twiga Stars) 2019.
Akiongea kuhusu kuwekeza katika
mpira wa vijana Bw. Malinzi alisema kuwa Msingi mkubwa wa mafanikio ya
timu za taifa duniani kote ni kuwekeza katika mpira wa vijana ili
kuhakikisha wanafundishwa mpira kwa kiwango cha kimataifa katika umri
mdogo utakaowasaidia kuwa imara.
Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) ulirasimishwa rasmi katika Mkutano Mkuu wa TFF wa
mwaka 2015 hivyo mfuko huo upo katika katiba ya TFF huku jukumu lake
kubwa ikiwa ni kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vitasaidia
Shirikisho hilo katika kutekeleza kazi zake mbalimbali za maendeleo ya
mpira wa miguu nchini.
0 comments :
Post a Comment