VIDEO: Nje ya Mahakama kuu baada ya kesi ya Mbowe, Wema Sepetu pembeni


Kutoka Mahakama kuu Dar es salaam leo jioni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea baada ya kutoka Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa DSM na Kamshna Sirro.
Tundu Lissu amewaambia Waandishi wa habari kwamba Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi March 2 2017, zaidi unaweza kumtazama Tundu Lissu hapa chini..
Pamoja na hayo, Mwigizaji Wema Sepetu alikuwepo Mahakamani hapo toka asubuhi ambapo ameonekana jioni hii akiwa pembeni ya viongozi wa CHADEMA na baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA walionekana kumkaribishwa kwa maneno wakati akiingia kwenye gari, hii video hapa chini itakuonyesha
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment