Mchungaji Josephat Gwajima ni mmoja wa watu waliotengeneza vichwa vya
habari wiki hii baada ya kutajwa kwenye orodha ya pili ya mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam ya watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye biashara ya
madawa ya kulevya.
Gwajima anafahamika kwa utajiri mkubwa kiasi cha kumiliki ndege,
helikopta na kudai kuwa na mpango wa kununua treni. Utajiri wake umekuwa
ukizusha maswali mengi na kupitia mkutano wake na waandishi wa habari
Alhamis hii uliofanyika kanisani kwake, Gwajima alielezea vyanzo vyake
vingine vya mapato.
“Cha kwanza mimi ni daktari wa philosophy, ni lecturer peke yake
Tanzania kwa malecturer wa kidini ambaye husafiri kwenda kulecture nje
ya nchi,” alisema.
“Lecture yangu moja nalipwa dola elfu moja, ambayo ni sawa sawa na
milioni 2 na laki kama nne, moja ya saa moja. Nikienda kulecture Japan
naweza kulecture miezi mitatu na mimi sijawahi kusafiri na hela mfukoni,
hela zote zinakuja kwa benki mpaka hapa. Chini ya kanisa letu kuna
kampuni zinaitwa Mahanai Organisations, ni makampuni makubwa.”
0 comments :
Post a Comment