Vodacom wamemkabidhi beki huyo wa Simba hundi ya Tsh milioni moja kama zawadi ya mchezaji bora wa mwezi December, baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, AyoTV ikafanya exclusive interview na Method Mwanjale ambaye amekiri kuwa ni kwa mara ya kwanza kufanya interview toka ajiunge na Simba.
“Kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Vodacom ni kitu kikubwa lakini mwisho wa siku mimi mipango yangu ni kushinda mataji na timu na sio tuzo binafsi, Ligi ya Vodacom ina changamoto nyingi sana unajua ina timu ngumu na zinaushindani ucheze na Simba, Yanga au Mbao FC zote ni imara”


0 comments :
Post a Comment