Bado haijajulikana kama kocha huyo ataendelea na Arsenal au kuachana nayo baada ya maneno hayo kuzidi, lakini habari zisizo rasmi kupitia mitandao mbalimbali ya soka iliripoti kuwa kocha huyo ameongezewa mkataba mpya wa miaka miwili.
Maneno yamekuwa mengi zaidi baada ya kipigo cha 5-1 walichokipata usiku wa February 15, hususani ulinganisha na hasira zao ambazo zimeongezeka baada ya kushindwa kutwa taji la Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 10 sasa ambapo mara ya mwisho ilikuwa 2003/2004, leo Wenger amenukuliwa na mitandao kadhaa akitoa kauli hizi.
"Hata kama nikiondoka sio kama watashinda kila mechi" >>> Arsene Wenger
"Nitaendelea kufundisha soka msimu ujao iwe Arsenal au sehemu nyingine yoyote" >>> Arsene Wenger


0 comments :
Post a Comment