Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limefikia makubaliano na
Kampuni ya Dangote Group of Industries kuhusu bei ya mauzo ya gesi
asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda chake cha saruji kilichopo
mkoani Mtwara.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TPDC, Kapulya Musomba alisema makubaliano hayo yanahusu kuunganisha
miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa kwenda
kiwandani hapo na kukamilisha mkataba wa awali kwa ajili ya mauzo ya
gesi kwa matumizi ya kiwanda hicho.
Alisema
makubaliano hayo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli. Desemba
mwaka jana, Rais Magufuli alipokutana na mmiliki wa kiwanda hicho,
Aliko Dangote jijini hapa alimtaka kununua gesi moja kwa moja kutoka
TPDC badala ya kutumia watu wa kati wenye nia ya kutengeneza faida
binafsi.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Dangote, Sada Ladan-Baki alisema gharama za kuunganisha
bomba hadi kiwandani zitabebwa na kampuni hiyo na siyo Serikali ya
Tanzania.
“Tutagharamia ujenzi wa bomba, mwanzo hadi mwisho na tutaanza ujenzi mwezi ujao,’’ alisema.
Alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kununua gesi nchini akisema hatua hiyo itatoa ajira kwa Watanzania wengi.
0 comments :
Post a Comment