Yanga Yatolewa Mashindano Ya Klabu Bingwa Afrika Na Zanaco


Michuano ya Club Bingwa Afrika hatua ya pili imeendelea leo kwa michezo kadhaa kuchezwa, Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar es Salaam Young Africanswalikuwa Lusaka Zambia katika uwanja waTaifa wa Mashujaa kuwania nafasi ya kuingia hatua ya makundi kwa kucheza dhidi yaZanaco.
Yanga ambao mchezo wa kwanza ulichezwaDar es Salaam na kulazimishwa sare ya 1-1, waliingia Zambia wakiwa na lengo moja la kuhakikisha wanasonga mbele hatua inayofuata kwa kupata ushindi katika mchezo huo au sare ya kuanzia 2-2 na kuendelea.
Sare tasa ya 0-0 inaiondoa Yanga katika michuano ya Club Bingwa Afrika dhidi yaZanaco kwa kujikuta game ikimalizika kwa sare tasa, hivyo Yanga sasa anaangukia katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kutolewa kwa kuruhusu kufungwa goli nyumbani katika mchezo wa kwanza uliyomalizika kwa sare ya 1-1.


:)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment