Shirikisho la vyama vya soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limezilalamikia nchi nne wanachama kwa kushindwa kusimamia kufanyika kwa mashindano ya Chalenji na Kombe la Kagame kwa miaka miwili mpaka sasa.
Katibu mkuu wa (CECAFA) Nicholas Musonye, amesema Nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ndizo zinazorotesha Michezo katika ukanda huu.
Amedai kuwa mtafaruku wote huu umezuka baada ya Uchaguzi wa CECAFA wa 2015 ambapo Rais wa Chama cha Soka cha Sudan, Muatasim Gafe, alipochaguliwa kuwa Mkuu wa CECAFA.
Amedai kuwa zipo siasa nyingi miongoni mwa wanachama ambao ni 12 na kusababisha baadhi ya wanachama kushindwa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika(AFCON).
Amedai kuwa zipo siasa nyingi miongoni mwa wanachama ambao ni 12 na kusababisha baadhi ya wanachama kushindwa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika(AFCON).
0 comments :
Post a Comment