Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mwanza imemkamata, James Mwansyemela kwa kosa la kujifanya mhandisi wa jiji na kushawishi kupokea rushwa ya Shilingi Laki Mbili kutoka kwa mfanyabiashara wa pembejeo za Kilimo aliyeingilia eneo la hifadhi ya barabara kinyume cha sheria.
Mwandishi wetu Innocent Aloyce anatuarifu kuwa, kwa mujibu wa Mkuu wa Takukuru mkoani humo, Ernest Makale, mtuhumiwa huyo anayetarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni, aliomba kiasi cha shilingi Milioni Moja, kwa mfanyabiashara huyo ili mpatie kibali cha kuendelea kufanyabiashara zake katika eneo hilo.
Hata hivyo mfanyabiashara huyu aliwaarifu Takukuru na ndipo alipowekewa mtego ambao ulikumba Mtendaji wa Kata ya Mkolani, Godfrey Mwang’onda aliyekiri baadaye kuagizwa na mtuhumiwa James Mwansyemela.
Hata hivyo kiongozi huyo wa Takukuru amesema katika uchunguzi waliofanya wamebaini kuwa, mtuhumiwa James Mwansyemela ni mzoefu wa matukio hayo baada ya kukutwa na vielelezo vinavyoashiria tayari alishawahi kushtakiwa kwa makosa kama hayo zikiwepo pesa taslimu Shilingi milioni moja na elfu hamsini ambazo mtuhumiwa alishindwa kutoa maelezo ya alikozipata.
Mtuhumiwa huyo alipozungumza na waandishi mara baada ya kuwekwa chini ya Ulinzi, amedaiwa kushangazwa na namna alivyoingizwa katika tukio hilo.
0 comments :
Post a Comment