Mzimu wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa umelitikisa tena Bunge baada
ya kutajwa kwa mara nyingine na wabunge wakati wakichangia bajeti kuu ya Serikali kwaKuondolewa kwa jina hilo kulizua zogo miongoni mwa wana CCM jambo ambalo lilifanya baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kuimba ‘Tuna imani na Lowassa’.

Jina hilo limebaki kuwa midomoni mwa wabunge wa CCM hata baada ya Lowassa kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema. Mijadala mingi inayowasilishwa bungeni imekuwa haipiti bila kutajwa kwa jina la mbunge huyo wa zamani wa Monduli.
Jana, kwa mara nyingine jina la Lowassa liliibuka baada ya Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara maarufu kama Bwege kumpa taarifa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Kiteto
Koshuma wakati akichangia hotuba ya bajeti.
Kiteto alimpongeza Rais John Magufuli na kusema kuwa kiongozi huyo ni fahari ya Watanzania
na ya wanachama wa CCM.
Koshuma wakati akichangia hotuba ya bajeti.
Kiteto alimpongeza Rais John Magufuli na kusema kuwa kiongozi huyo ni fahari ya Watanzania
na ya wanachama wa CCM.
“Rais ni fahari ya mataifa mbalimbali, ni fahari kwa dunia nzima mambo ambayo anayafanya
Rais anastahili kupewa pongezi kama yeye, hata mimi najisikia fahari kutembea na nguo zangu
za rangi ya kijani kwa sababu ya mazuri anayofanya Rais,” alisema na kuongeza:
Rais anastahili kupewa pongezi kama yeye, hata mimi najisikia fahari kutembea na nguo zangu
za rangi ya kijani kwa sababu ya mazuri anayofanya Rais,” alisema na kuongeza:
“Kuna mbunge alidiriki kusema kuwa ni Serikali ya Magufuli. Hapana sio kwamba alisema kuchagua Serikali ya Awamu ya Tano ni ya Magufuli bali alitaka tumwamini yeye kama mtu.”
Hata hivyo, Bungara aliomba kutoa taarifa kwamba yeye ndiye aliyewahi kusema kuwa Serikali ni ya Magufuli.
“Naomba niulize hivi kabla ya Magufuli kuwa Rais, asimame mmoja tu ambaye alikuwa akimuunga mkono Magufuli kabla ya Lowassa kutolewa (kwenye mchakato wa uchaguzi CCM).

Kwa hiyo hii ni Serikali ya Magufuli sio ya CCM,” alisema Bwege.
Baada ya kauli hiyo walisimama wabunge kama 10 hivi wa CCM wakionyesha kuwa walikuwa
wakimuunga mkono Magufuli na hawakumuunga mkono Lowassa akiwa CCM.
wakimuunga mkono Magufuli na hawakumuunga mkono Lowassa akiwa CCM.
“Waongo nyinyi wote wanafiki tu. Tuna imani na Lowassa mliimba nyote, nyinyi wahuni nyinyi,”
alisema na kuzua minong’ono miongoni mwa wabunge ambao baadhi yao walisikika wakiimba
“Tuna imani na Magufuli.”
alisema na kuzua minong’ono miongoni mwa wabunge ambao baadhi yao walisikika wakiimba
“Tuna imani na Magufuli.”
Baada ya hayo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alimruhusu Kiteto kuendelea kuchangia lakini akaikataa taarifa ya Bungara. “Na siwezi kuikubali na ndio maana nilianza na utangulizi wa kuongelea ibara ya nane ya Katiba, Lowassa alikuwa mtendaji na atawajibika kama mtendaji, mimi sitaki kuhesabu yaliyopita nataka kusonga mbele,” alisema Kiteto wakati akiendelea kuchangia
Kabla ya tukio la jana, mzimu wa Lowassa umewahi kuibuka katika matukio mbalimbali likiwamo la Julai 23, 2016 wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alipokumbushia kilichotokea katika kikao cha Halmashauri Kuu mwaka 2015 baada ya jina la Lowassa kuenguliwa.
Pia, alikumbushia jinsi ambavyo wana CCM walivyoimba “Tuna imani na Lowassa” wakati jina
lake lililipokatwa.
lake lililipokatwa.
Kadhalika Januari, 2016 jina la Lowassa liibuka tena bungeni baada ya mbunge Hafidh Tahir
kuishauri Serikali ibadili sheria ili viongozi wa zamani wa kitaifa wasipewe stahiki zao pindi wanapohamia vyama vingine.
kuishauri Serikali ibadili sheria ili viongozi wa zamani wa kitaifa wasipewe stahiki zao pindi wanapohamia vyama vingine.
Tahir alimrejelea Lowassa ambaye ni waziri mkuu mstaafu aliyehamia upinzani.
Mwezi Aprili jina la Lowassa liliibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki
(Chadema), Joshua Nasari alipouhoji utendaji wa Waziri wa Katiba na Sheria (wakati huo), Dk Harrison Mwakyembe ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond.

Nasari alihoji ni kwa nini Dk Mwakyembe hakumhoji Lowassa katika sakata la kuzalisha umeme
wa dharura baina ya Tanesco na Richmond Development.
wa dharura baina ya Tanesco na Richmond Development.
Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema wapinzani wanataka kumsafisha Lowassa na kuongeza kuwa hakuona haja ya kumhoji kwa kuwa ushahidi ulikuwa wazi. Waziri huyo alikwenda mbali zaidi na kusema, wapinzani wakitaka suala la Lowassa lirudi bungeni yuko tayari kuvuliwa uwaziri ili alishughulikie.
Alipoulizwa katika viwanja vya Bunge anazungumziaje wabunge wa CCM kusimama kuonyesha
kuwa walimuunga mkono Dk Magufuli kabla ya Lowassa kujitoa katika uchaguzi, Bungara
alisema, “Waongo wanajua kuwa walikuwa wanamuunga mkono Membe (Bernad Membe
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) lakini baada ya jina
kuondolewa ndipo walimuunga mkono Magufuli.

0 comments :
Post a Comment