Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali imekiri kuelemewa na matukio hasa sampuli za jinai ambazo ni nyingi
ikilinganishwa na idadi ya watumishi waliopo nchi nzima ambao ni 190 tu wakati mahitaji kwa kuanzia ni watumishi 400 ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi.
ikilinganishwa na idadi ya watumishi waliopo nchi nzima ambao ni 190 tu wakati mahitaji kwa kuanzia ni watumishi 400 ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi.
Mkemia Mkuu wa serikali Prof. Samwel Manyelle ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tuzo kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka jana na kufanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biology ambapo amesema kwa mwaka sampuni za jinai peke yake ziko 60,000 huku maeneo ya bandarini na mipakani kukihitaji watumishi wa kutosha.
Akizungumza na wanafunzi hao Mganga mkuu wa serikali Prof Mohamad kambi ambaye alikuwa mgeni rasmi ameahidi kushirikiana na ofisi hiyo katika kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi kwani ni ofisi muhimu hasa ikizingatiwa kuwa serikali ya awamu ya tano msisitizo wake ni kukuza uchumi wa viwanda.
Baadhi ya wanafunzi waliopata tuzo hizo wamesema tatizo kubwa linaloikabili masomo ya sayansi kwenye shule nyingi hasa za serikali ni ukosefu wa maabara ambazo zitawasaidia wanafunzi kusoma kwa vitendo na kuiomba serikali kuongeza kasi ya kuhakikisha kila shule ya sekondari inakuwa na maabara.
0 comments :
Post a Comment