Uzinduzi wa mtandao wa wabunge wa kufuatilia bajeti
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamezindua mtandandao maalumu wa kibunge utakaowajibika kufuatilia na kufanya tathimini ya utekelezaji wa bajeti za serikali.
Mtandao huo uliozinduliwa hii leo mjini Dodoma na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Paramagamba Kabudi, unajumuisha wabunge wanachama 100 huku ukifadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB .
Akizungumza baada ya uzinduzi huo ulioambatana na mafunzo maalum kwa wabunge wanachama, Prof. Kabudi amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kubadilisha mijadala ndani ya Bunge na kuwa mijadala yenye tija badala ya mijadala ya mipasho na malumbano.
Nao wabunge ambao ni wanachama wa mtandao wamesema kuwa mtandao huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kutambua na kuhakikisha kuwa miradi yote iliyomo kwenye bajeti inatekelezwa huku wakivua ‘ngozi’ za vyama na kuwa kitu kimoja.
Tanzania ni nchi pekee katika nchi wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki ambayo haikuwa na mtandao huoFacebook