Idara ya uhamiaji nchini inawashikilia watu watano wakiwemo Afisa polisi mstaafu na mtumishi wa halmashauri ya jiji mstaafu wakiwa na nyaraka mbalimbali za serikali za kugushi na mihuri 50 tofauti tofauti ya ofisi za serikali na mawakili.
Kamishina wa Usimamizi na udhibiti wa mipaka bw Samuel Magweiga amesema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Salaam wakiwa katika ofisi alizodai kuwa wanafanyia utapeli huo wakiwa na nyaraka hizo na kuongeza kuwa upelelezi umekamilika na watafikishwa mahakamani.
Kati ya nyaraka ambazo watuhumiwa hao wamekutwa nazo ni pamoja na vyeti vya kughushi vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam na katika hali isiyokuwa ya kawaida watuhumiwa hao wakati wanahojiwa na waandishi wa habari wakiwa katika ofisi za makao makuu ya idara hiyo wamekana kutokuhusika na ofisi hiyo huku kila mmoja akidai kuwa alipitia ofisini hapo kusalimia.
CHANZO ITVFacebook