Mbunge Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa leo kwa gazeti la MAWIO, asema hatua hiyo inawanyima Wananchi mawazo mbadala ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa facebook.
ZITTO KABWE:Uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli Mwenyewe sio Mawio.
Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake.
Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais.
Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.
Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.
Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.
Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu.
na kumalizia kwa hashtag ya #PressFreedom #UhuruWaHabari

0 comments :
Post a Comment