Mshambuliaji Ibrahimu Ajibu amesaini rasmi mkataba wa kujiunga na klabu ya Yanga akitokea kwa mahasimu wao Simba SC.
Nyota huyo aliyeng’ara zaidi akiwa na Wekundu wa Msimbazi, ametambulishwa rasmi leo na uongozi wa Yanga na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa ikitumiwa na Matheo Anthony.
Akizungumza katika tukio hilo, Ajibu ameahidi kuitumikia Yanga kwa uaminifu na kwa kiwango zaidi ya kile alichokuwa nacho Simba.
Hatua hiyo inazima rasmi tetesi zilizokuwepo juu ya usajili wa mshambuliaji huyo, ambapo palikuwa na taarifa za muda mrefu kuwa huenda kipenzi huyo wa wana Msimbazi akahamia upande wa pili.
0 comments :
Post a Comment