Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwapa taarifa wadau wetu hususan waombaji kazi waliokuwa wameshawasilisha maombi na wale ambao watapenda kuwasilisha maombi ya kazi kwa nafasi zilizotangazwa na chombo hiki kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwa kuna mabadiliko yamefanywa na mamlaka husika (TRA) ambapo nafasi za kazi mia moja (100) zilizokuwa zikiwahitaji (ESTATE OFFICER II) hazitakuwepo tena na badala yake watahitajika (REVENUE OFFICER II -100).
Hivyo, wale waombaji ambao walikwishawasilisha maombi yao kwa nafasi hiyo, watapaswa kuyawasilisha upya na kuzingatia sifa zilizoainishwa katika tangazo lenye Kumbukumbu namba EA.7/96/01/149 lililoko kwenye tovuti www.ajira.go.tz ambalo mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19 Julai, 2017.
Tunapenda kuwaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na mabadiliko hayo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira
ANGALIZO KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitizia waombaji kazi wote kusoma kwa makini tangazo la nafasi za kazi na kuzingatia sifa za msingi na maelekezo yaliyotolewa kabla ya kutuma maombi ikiwemo kuthibitisha (Certify) Nyaraka (Vyeti) pamoja na kuweka sahihi (Signature) katika barua ya maombi ya kazi ambayo imeainisha nafasi inayoombwa.

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki katika “Recruitment portal” http://portal.ajira.go.tz ya Sekretarieti ya Ajira. Watakaoenda kinyume na malekezo hayo, maombi yao hayatashughulikiwa.
Imetolewa na; Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
0 comments :
Post a Comment