AJIRA MPYA:Serikali yatangaza vigezo vya kuajiri watumishi wapya na mgawanyo wake

Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia mgawanyo sahihi wa rasilimali watu katika Utumishi wa Umma ili kuwa na utendaji bora na wenye matokeo katika utumishi wao.
Ameyasema hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki katika kikao kazi na watumishi wa umma wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Kairuki amesema mwajiri anapoomba kibali cha kuajiri watumishi ni vyema akazingatia mahitaji kulingana na majukumu yaliyopo ili kuondoa ziada ya watumishi wa umma wasio na kazi kuendana na fani walizosomea kwa lengo la kuwa na utendaji mzuri.
“Ni vizuri wakati tunaomba vibali vya kuajiri watumishi wa umma tukazingatia mgawanyo sahihi wa rasilimali watu katika maeneo yetu kulingana na majukumu ya watumishi tunaowahitaji badala ya kuomba watumishi wengi ambao wanasababisha kuwa na ziada ambayo haitumika ipasavyo,”amesema waziri Kairuki.
Waziri Kairuki amesema katika vibali 10,184 vilivyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, halmashauri ya manisapaa ya Ubungo imetengewa jumla ya nafasi 140.
Ameongeza kuwa, halmashauri hiyo imetengewa jumla ya nafasi za ajira mpya 397 kwa mwaka wa fedha 2017/18 hivyo zitendewe haki kwa kuhakikisha watumishi watakaoajiriwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mpango uliopo.
Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Dar es salaama kwa lengo la kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika utumishi wa umma ili kufikia malengo yaliwekwa Serikali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment