JUMUIYA ya Tawala ya Mitaa (ALAT) Tanzania inatarajia kuhamia mkoani Dodoma ifikapo tarehe 1 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuzitaka serikali kuhakia mkoani humo, anaandika Catherine Kayombo.
Mwenyekiti wa ALAT taifa, Gulam hafeez Mukadam, ametoa taarifa hiyo katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo idara ya habari na maelezo jijini Dar es salaam.
“Naunga mkono juhudi za rais kwa vitendo kwa kuhamishia shughuli za serikali makao makuu Dodoma, ambapo ALAT kuanzia tarehe mosi Agosti, 2017 ofisi za makao makuu zitahamia Dodoma”, alisema Mukadamu.
Katika mkutano huo, mwenyekiti pia amekemea watumishi wa ALAT wasio waadilifu na kutoa taarifa ya hatua zitakazochukuliwa ili kuhakikisha kurejesha amani kwa wanajumuiya.
“Hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watumishi wa sekretariat ya ALAT makao makuu ambao siyo waadilifu na wenye utendaji kazi usioridhisha”, aliongeza.
Mukadamu ametoa rai kwa mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuchangia chombo chao cha ALAT kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa manufaa ya wananchi.
0 comments :
Post a Comment