BAKWATA YAITAKA SERIKALI KUMCHUKULIA HATUA MTU MMOJA ANAYEJIITA MTUME MKOANI PWANI.

Baraza la ulamaa limetoa wito kwa vyombo vya dola kumchukulia hatua stahiki mtu aliyejitokeza katika mkoa wa pwani na kudai yeye ni Mtume.
Akisoma wito huo, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Hamisi Said Mataka amesema, anachodai mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Hamza Issa kuwa yeye ni nabii hayako kabisa katika mafundisho ya kiislamu.
Amesema kauli ya Issa kudai yeye ni mtume na kisha kwamba ni Muislamu kwa kutumia maandiko ya Uislamu, ni upotoshaji mkubwa ambao ukiachwa bila kudhibitiwa ni kuruhusu fujo na uvunjifu wa amani.
“Kwa mujibu wa maelezo yaliyoenea katika mitandao ya kijamii na ya kutoka baraza za Masheikh wa Mkoa wa Pwani chini ya kiongozi wake Sheikh na Qadhi wa Mkoa wa Pwani, amedai kuwa yeye ni Nabii Ilyasa kwa maana ya kwamba roho ya Nabii Ilyasa imemuingia yeye Hamza Issa na kwa hiyo yeye amekuwa Nabii Ilyasa” amesema Sheikh
Ameongeza maelekezo na mafundisho ya uislamu yako wazi kuwa hakuna Mtume mwingine katika Uislamu baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) na kwamba upatikanaji wa MTU ndani ya uislamu na kudai kuwa yeye ni Mtume ni kutaka kuamsha hisia Kali za waislamu nchini.
“Baraza la Ulamaa linapenda kuwafahamisha waislamu kwamba, yeyote atakayemfuata mpotoshaji huyu atakuwa ametoka ndani ya uislamu” amesema Sheikh Mataka.
Pia Baraza limetoa wito kwa Masheikh wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa taasisi mbali mbali za Kiislam kutotoa fursa ya aina yoyote kwa huyo anayejiita Nabii ( Hamza Issa), ili kuzuia kuipotosha jamii.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment