Hatimaye klabu ya Man United imemsajili na kumsainisha straika Romelu Lukaku mkataba wa miaka mitano akitokea Everton.
United imesajili mshambuliaji huyo ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Chelsea, kwa dau la awali la pauni milioni 75 ambapo taarifa zinasema kuwa uhamisho huo utakuwa na nyongeza ya pauni milioni 15.
Meneja wa Man United Jose Mourinho amemmwagia Lukakau misifa akisema kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ni mchezaji sahihi kwa klabu yake kwa kuwa ni mchezaji mkubwa duniani kwa sasa.
“Ni jambo lisiloweza kuzuilika kwamba Lukaku anataka kuendeleza fani yake katika klabu kubwa, ni ongezeko muhimu katika klabu hii. Natamani sana kufanya naye kazi tena” Amesema Mourinho ambaye aliwahi kuwa kocha wake wakati alipokuwa Chelsea.
Kwa upande wake Lukaku amefurahi kwa hatua ya kujiunga na Man United na ndiyo maana siku waliposema kuwa wanamuhitaji, hakujifikiria mara mbili kwa kuwa aliona kuwa hiyo ni fursa adhimu katika maisha yake.
Siwezi kufikiria kuikwepa Old Trafford mbele ya mashabiki zaidi ya 75,000” amesema Lukaku ambaye mkataba wake una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
0 comments :
Post a Comment