Madiwani Chadema Arusha watawaliwa ‘umalaya’ wa kisiasa


WIMBI la viongozi wa vyama vya upinzani mkoani Arusha kujiuzulu limeendelea kushika kasi baada ya Diwani wa Viti maalumu (CHADEMA ) wilaya ya Ngorongoro, Manda Ngoitika naye kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo, anaandika Mwandishi Wetu.
Diwani huyo ambaye pia ni Mwanaharakati anayejihusisha na utetezi wa kisheria wa masuala ya wanawake wa jamii za wafugaji amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa hakuna sababu ya kuwa mpinzani wakati yale yote aliyokuwa anayapinga sasa yanafanyiwa kazi.
Pia alisema kuwa kwa sasa licha ya kuendelea kukiunga chama cha mapinduzi mkono na serikali yake anajikita zaidi kwenye shughuli za harakati za kutetea jamii hasa za wafugaji ambazo bado zinakabiliwa na matatizo mengi.
“Kulingana na sheria za sasa ambazo zinakataza mtu kuwa na NGO’s na pia kujihusisha na siasa nimeona nianza kujiimarisha kwenye masuala ya utetezi wa jamii zaidi “alisema Manda Ngoitika -Mwanaharakati.
Amesema ameona kuwa siyo vizuri kuendelea kuwa mnafiki wa kuonyesha kuwa yupo upinzani wakati hana anachopinga na kwamba ameona ni bora awe wazi na dunia ijue kuwa sasa yeye anaunga mkono yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe magufuli.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Raphael Siumbu, amethibitisha kupokea barua ya diwani huyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Bw, Methew Siloma amesema kiongozi huyo alitangaza kujiuzulu kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani mbele ya Madiawani wenzake
Kuhusu tuhuma zinazotolewa za kuwepo kwa ushawishi wa fedha wa kuwafanya viongozi hao kujiuzulu, Siloma alisema kuwa hayana msingi kwani hakuna mtu mwenye pesa za kuchezea na pia hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Aidha, Siloma aliwataka wanaolalamika na kueneza maneno ya kuwepo kwa ushawishi wa fedha kutambua kuwa upepo wa kisiasa na hauzuiliki na hata wanasiasa wanajua hivyo wakubali matokeo na waache kutafuta mchawi.
Wimbi la madiwani wa chadema wa mkoa wa Arusha kujiuzulu lilianzia katika wilaya ya Arumeru na sasa limekuwa likieneo katika maeneo mengine ikiwemo wilaya ya Arusha . Monduli na sasa Ngorongoro
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment