JESHI la Polisi mkoani Mbeya kwa kushirikiana na askari wa TANAPA wamekamata pikipiki sita zikiwa zimepakia nyara za serikali katika pori la hifadhi ya Taifa la Ruaha liliopo katika kijiji cha Nyamlala tarafa ya Rujewa wilayani Mbarali, anaandika Mwandishi Wetu.
Nyara zilizokamatwa ni pamoja na ngozi moja ya simba na vipande 15 vya meno ya tembo vikiwa vimepakiwa katika pikipiki hizo huku zikiwa zimetekelezwa na wahusika ambao walikimbia.
Tukio hilo limetokea baada ya kuwapo msako mkali wa jeshi la polisi na askari wa TANAPA katika hifadhi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya , Mohammed Mpinga amesema baada ya pikipiki hizo kukamatwa wahusika walikimbia na kuzitekeleza katika pori hilo.
Kamanda Mpinga amesema kati ya pikipiki hizo, mbili zilikuwa hazina namba za usajili huku nyingine zikiwa ni MC 386 BHW aina ya Kinglion, MC T.799 CTW aina ya T-Better, MC 755 ADJ, T.461 BZE.
Aidha, Mpinga amesema pikipiki hizo baada ya kukaguliwa zilikutwa na nyara za serikali ambazo ni ngozi moja ya Simba na vipande 15 vya meno ya Tembo.
“ Upelelezi na ufuatiliaji unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hili ili waweze kuchukukuliwa hatua zinazostahili”amesema Kamanda Mpinga.
0 comments :
Post a Comment