Malinzi Na wenzake waendelea kusota rumande

KESI inayomkabiri Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi,Katibu wake Celestine Mwesigwa na Mtunza Fedha,Nsiande Mwanga imesoma tena leo asubuhi kwenye mahakama ya Kisutu,Dar Es Salaam.

Imeamuliwa kuwa Malinzi pamoja na wenzake warejeshwe tena rumande kwa madai kuwa upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika na watarejeshwa tena mahakamani hapo Julai 30 mwaka huu.

Malinzi anakabiriwa na mashitaka 28 ya kughushi nyaraka na kutakatisha fedha wakati Mwesigwa na Mwanga wanakabiriwa na mashitaka matatu kila mmoja.

Malinzi na wenzake walifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza Juni 29 kabla ya kupandishwa tena kizimbani Julai 3 mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment