Mkuu wa mkoa wa Geita amemzuia naibu waziri wa habari,sanaa utamaduni na michezo Wambura kuzindua Filamu ya Magwangala kwa madai ya kuwa na maudhui yanayodaiwa kuutia doa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema uamuzi wa kuagiza kuahirishwa kwa uzinduzi huo
ulichukuliwa na mkuu wa mkoa, Ezekiel Kyunga ili kutoa fursa ya kusikiliza hoja na malalamiko kutoka GGM baada ya kubainika kuwa sehemu ya maudhui ya filamu inaigusa kampuni hiyo kwa taswira hasi.
ulichukuliwa na mkuu wa mkoa, Ezekiel Kyunga ili kutoa fursa ya kusikiliza hoja na malalamiko kutoka GGM baada ya kubainika kuwa sehemu ya maudhui ya filamu inaigusa kampuni hiyo kwa taswira hasi.
Wambura alifika Geita mchana wa Julai 27 tayari kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyochezwa na wasanii wa mkoani hapa wakiwamo Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji wa Geita, Leonard Bugomola ambao ulipangwa kufanyika saa moja usiku katika
ukumbi wa Desire Park.
Halmashauri ya Mji wa Geita, Leonard Bugomola ambao ulipangwa kufanyika saa moja usiku katika
ukumbi wa Desire Park.
Filamu hiyo inaelezea maisha ya wachimbaji wadogo wanavyotegemea magwangala. “Nilifika kwa mkuu wa mkoa kama mwenyeji wangu ndipo nikapata taarifa kuwa GGM wamelalamikia picha (filamu) kuwa si nzuri kwao. Tulikaa kujadili lakini hatukufikia mwafaka ndiyo maana leo (juzi) asubuhi nimeamka kuingia kwenye kikao kati ya mkuu wa wilaya, wasanii na mwakilishi wa GGM,” alisema.
Katika mazungumzo hayo, naibu waziri alisema GGM walitishia kwenda mahakamani. Hata hivyo, hakufafanua zaidi huku akisema amegundua kwamba kuna tatizo kubwa kati ya ofisa utamaduni na bodi ya filamu; ofisa utamaduni na mkuu wa mkoa; na pia ofisa utamaduni na wasanii.
“Kutokana na hali hiyo, ndiyo maana niliacha kuizindua ili tumalize kwanza haya mambo na wananchi wasiwe na wasiwasi tutakuja tena kwa ajili ya kuizindua,” alisema naibu waziri.
0 comments :
Post a Comment