Wanaokiuka agizo la Rais kuhusu Elimu bure waonywa.

Nkupamah media

download (10)Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Serikali imewaonya wadau wa elimu nchini  wanaoendelea kutoza wanafunzi fedha za kwa ajili ya kujisajili pamoja na michango mbalimbali waache mara moja.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Ufundi  Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu agizo la elimu bila malipo kwa Shule zote za Umma pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.
“ Napenda kusisitiza kuwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ,Miji na Manispaa zote nchini wafuatilie kwa karibu utekelezaji wa agizo hilo na watoe taarifa za Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule watakaokwenda kinyume ili hatua stahiki zichukuliwe” Alisema Mhandisi Manyanya.
Pia Mhandisi Manyanya ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa katika Ofisi za Elimu zilizopo katika maeneo  yao  pale wanapobaini kuwa kuna shule zinakiuka agizo hilo.
Akijibu swali kuhusu suala la ada elekezi Kamishna wa Elimu Prof Eustella Bhalalusesa alisema kuwa ataitisha kikao na wamiliki wa shule binafsi kujadili  kuhusu utozaji wa ada ambazo zitakuwa na unafuu  kwa wananchi
.
Aidha Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu ya Juu Bw. Jonathan .S. Mbwamba  amesisitiza kuwa kila mwanafunzi mwenye sifa atapata mkopo na kuongeza kuwa  idadi ya wanafuzi wanaopata mkopo imefikia wanafunzi 53,032 kutoka kwenye lengo lililowekwa la kuwapatia mkopo wanafunzi 13,582.
Kuanzia mwaka wa masomo 2016, elimu katika shule za Umma itatolewa bure kupitia Waraka namba 5 wa mwaka 2015 kuhusu utoaji wa elimu pasipo  malipo na Waraka namba 6 wa mwaka 2015 ambao ulitoa ufafanuzi na melekezo ya utekelezaji wake
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment