Mbwana Samatta ameanza msimu wa ligi ya Ubelgiji kwa kufunga goli moja kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo wakati Genk ikicheza dhidi ya Waslaand Beveren kwenye uwanja wa nyumbani wa Genk.
Katika mchezo huo, timu ya Samatta imelazimishwa sare ya kufungana 3-3 ikiwa ni mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ya Ubelgiji 2017/2018. Magoli ya Genk yamefungwa na Jose Naranjo dakika ya 70, Mbwana Samatta dakika ya 80 na dakika ya 82 Shrivjers akafunga goli la mwisho.
Beveren wao walifunga magoli yao kupitia kwa Olivier Myny dakika ya 45, Zinho Gano dakika ya 47 na 90.
Unaweza kutazama magoli kwenye video hapo chini
0 comments :
Post a Comment