Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa mkoani Mbeya TAKUKURU imempandisha kizimbani Angelica Yohana Wavenza ambaye ni Afisa Manunuzi katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya akituhumiwa kutenda makosa ya ufujaji na ubadhilifu wa mali za umma.
Wavenza amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya akituhumiwa kutenda kosa la wizi wa mali za umma chini ya vifungu namba 265 na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Mbeya, Emmanuel Kiyabo amewaambia wanahabari ofsini kwake kuwa kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa No.11/2007 kinazuia mtumishi wa umma kutenda kosa la ufujaji wa mali za umma.
0 comments :
Post a Comment