Nyosso na wenzake waanza mazoezi makali Dar

Timu ya Kagera Sugar ya Bukoba leo asubuhi imeanza mazoezi katika Uwanja wa Karume ikiwa ni kambi yake ya awali jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza Agosti 26, mwaka huu.
Wachezaji wote wapya sita, wakiongozwa na beki maarufu wa zamani wa Simba, Juma Said Nyosso, anayerejea kwenye soka baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa miaka miwili, walikuwemo katika mazoezi hayo.
Nyosso akiwa Mbeya City mwaka 2015, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kufungiwa muda mrefu katika soka ya Tanzania baada ya kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu uwanjani.
Wachezaji wengine waliosajiliwa Kagera Sugar ni pamoja na Said Kipao, Peter Mwalyanzi, Omary Daga ‘Dagashenko’, Venance Ludovic pamoja na Japhary Kibaya
Kocha mkuu wa Kagera, Mecky Maxime aliyezungumza na kipindi cha Mshikemshike cha Azam TV, amesema kwa aina ya wachezaji aliowasajili anaaamini watafanya vizuri msimu ujao.
Msimu uliopita, Kagera Sugar ilimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Yanga walioibuka mabingwa na Simba washindi wa pili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment