Rais Magufuli ashutumiwa na ukabila

Rais John Magufuli akishuka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania
TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema amemvaa tena Rais John Magufuli na sasa amemshutumu kwa kuendesha nchi kwa misingi ya upendeleo wa kikabila na kikanda, anaandika Jovina Patrick.
Lissu amewaambia waandishi wa habari: “Nani anaweza kubisha kwamba Rais Magufuli anaendesha nchi kwa misingi ya upendeleo wa kifamilia, kikabila na kikanda?”
Mwanasheria huyo amesema kitendo cha Rais Magufuli kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato ni dhahiri kuwa umejengwa kwa upendeleo kwani hakuna anayejua bajeti yake wala kama ulikidhi vigezo vya kujengwa huko na siyo mikoa mingine.
Lissu amedai kuwa Rais amekuwa akiajiri na kuwapa nyadhifa za juu ndugu zake na watu wanaotoka kanda ya ziwa ili aendelee kuwa na nguvu kubwa ya kuwakandamiza wananchi wa chini.
“Mkuu wa majeshi msukuma, mkuu wa polisi anatoka kanda ya ziwa, mwanasheria mkuu wa serikali anatoka kanda ya ziwa. Anashikilia mpini alafu wananchi wa chini wanashikilia makali na wao ndiyo wanaoumia,” anasema Lissu.
Unaweza kutazama  Video hapo chini kusikia alichozungumza Tundu Lissu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment