MARA baada ya kuachiwa huru na mahakama, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ametupa dongo lingine kwa Rais John Magufuli kwa kumwambia kuwa watanyamaza wakiwa wafu, anaandika Hellen Sisya.
Lissu alipoachiwa na mahakama alienda moja kwa moja Makao Mkuu ya Chadema, ambako alikutana waandishi wa habari, katika mkutano huo pamoja na mambo mengine amesema: “Mwambieni Magufuli (Rais John Magufuli), tutanyamaza tukiwa wafu.”
Akiongea kwa kujiamini Lissu amesema, “wanataka tunyamaze ili waendeshe nchi hii wanavyotaka wao, Taifa hili ni la mfumo wa vyama vingi, tunayo haki ya kufanya mikutano, tunayo haki ya kufanya maandamano na tunayo haki ya kutoa maoni yetu. Kwa msingi huo hakuna wa kutunyamazisha, nchi hii siyo mali ya mtu binafsi.”
Amesema, “naomba niweke wazi kabisa. Hakuna gereza, wala mahabusu, wala polisi, wala usalama wa taifa, wala Magufuli na wala mtu yeyote atakayetunyamazisha. Narudia. “Hatutakubali kunyamazishwa. Kwa sababu, tukinyamaza kwa kuogopa mahabusu, tukaogopa magereza, tukaogopa mabomu ya mapolisi, tukanyamaza. Nchi hii, inaangamia.”
Kwa mujibu wa Lissu, hicho ndicho wanachotaka. Alisema, “wanataka tunyamaze ili waendeshe nchi wanavyotaka wao.”
0 comments :
Post a Comment