Twaweza Yaja Na Utafiti Mwingine


Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali.

UTAFITI uliofanywa na taasisi ya Twaweza umeonyesha kuwa usalama kwa nusu ya Watanzania umeimarika katika mwaka mmoja uliopita kwa asilimia 53 ambapo asilimia 37 walisema hali ya usalama imebaki vilevile na asilimia 10 wanasema hali imekuwa mbaya zaidi. 

Utafiti huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, katika mkutano na wadau uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar, alipofafanua kuwa matokeo hayo yametokana na utafiti wake uitwao ‘Hapa usalama tu: Usalama, polisi na haki nchini Tanzania’.


Mkutano na wadau ukiendelea.

“Muhtasari huu unatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka sauti za wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika kwenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mkononi.

Ni matokeo na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,805 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara bila kuhusisha serikali ya Zanzibar yaliyofanyika Aprili mwaka huu,” alisema.

YALIYOMO KWENYE RIPOTI YA TWAWEZA


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment