Ukosefu dawa tatu za tiba kuwafukuzisha kazi waganga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, amewaagiza waganga wakuu wa wilaya zote nchini kuhakikisha wanakuwa na dawa tatu za uzazi salama ili kutokomeza vifo vya kina mama na watoto.
Waziri Mwalimu ametoa agizo hilo jana Jumatatu Julai 17, wakati akikabidhi gari la wagonjwa na vifaa tiba mbalimbali ikiwemo mashuka na vitanda kwenye Kituo cha afya cha Pongwe kilichopo kata ya Pongwe, Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Mariam Shedafa, aliyeshuhudia tukio hilo, dawa zinazotakiwa kuwepo kwenye kila hospital ni zile za kuzuia mama mjamzito asivuje damu kabla na baada ya kujifungua na dawa ya kumuokoa mama ambaye amepata kifafa cha mimba.
Waziri huyo amesema mganga mkuu wa wilaya ambaye atakutwa hana dawa hizo, atapaswa kujiuzulu mara moja kwani atakuwa hatoshi kwenye nafasi yake kutokana na umuhimu wa dawa hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment