Wizara ya afya nchini imekanusha taarifa zilizoenea zikidai kuwa wanafunzi watakaoanza mafunzo kwa vitendo yanayofahamika kama mafunzo ya utarajali (Internaship programme) walio chini ya wizara hiyo kuanzia mwaka huu hawatapewa fedha za kujikimu.
Taarifa iliyotolewa leo na wizara hiyo kupitia kwa mkuu kitengo chake cha mawasiliano Nsachris Mwamwaja imeeleza kuwa kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwa kuwa bado inasubiri waliopo kwenye mafunzo, watoke ndipo ipangie wengine.
Mwamwaja amesema kuwa barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa mujibu wa sheria, hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.
Aidha amesema wapo ‘intern’ wawili wanaosoma nchini China na mwingine Algeria ambao masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikuwa ni lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo kwa kujigharimia wenyewe, ili warudi mapema kumalizia program yao ya udaktari.
“Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliopewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo”. Imefafanua taarifa hiyo
0 comments :
Post a Comment