Aliyeanzisha ‘Magufuli Baki’ akimbilia TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeombwa kufuatilia kwa makini mawasiliano ya simu za mkononi ili kubaini watu wanaotumia mitandao hiyo kinyume na sheria.
Ombi hilo limetolewa na mwanaharakati Lawrence Mabawa jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari vitisho anavyopata kupitia simu ya mkoni baada ya kutambulisha kampeni yake ya ‘BAKI MAGUFULI’.
Kwa mujibu wa Mabawa, baadhi ya wananchi wameelewa vibaya kampeni hiyo na kufikia hatua ya kutoa maneno ya matusi na kejeli kwake.
Akifafanua lengo la kampeni yake, Mabawa amesema alimaanisha kuwa Rais abaki na msimamo wake ambao kwa kiasi kikubwa unapeleka taifa la Tanzania mbele kimaendeleo, na si kama ambavyo watu hao wameichukulia
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment