Maonesho ya nane nane yadorora Dodoma


MAONESHO ya Wakulima ya nane nane mwaka huu yanayofanyika mkoani Dodoma yamedorora, anaandika Dany Tibason.
Baadhi ya washiriki waliozungumza na MwanaHALISI online katika maonesho hayo,walisema ni bora kuyafuta.
Walisema maonesho haya ya nane nane yamekuwa hayana tija kwa wakulima kutokana na watumishi wa serikali kutoyapa kipaumbele.
Mbali na hilo wengine walisema licha ya serikali kujinadi kwamba Tanzania uchumi wake unakua lakini Watanzania bado wana hali mbaya.
Mosses Mdulani mkazi wa mkoa wa Dodoma, alisema kuwa kwa sasa hali ya uchumi imekuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa hali ya chini jambo ambalo limesababisha wafanyabiashara wadogo kushindwa kufanya biashara.
”Awali tulikuwa tukifanya biashara ya kuuza nyama ya ng’ombe, angalau tulikuwa tunachinja ng’ombe watatu kwa siku na tunamaliza, lakini kwa sasa tunachinja ng’ombe mmoja na tunashindwa kumaliza nyama,” alisema
Mjasiliamali mwingine ambaye anajihusisha na ufugaji wa nyuki kutoka Chiboli wilayani Chamwino, Bahati Thadei, alilalamikia maandalizi mabovu na kusema kwamba yamesababisha maonesho kudorora.
“Tumejikuta katika banda hili la Chamwino tukiwa wawili tu hatujui halmashauri inawaza nini kwa maana hakuna maandalizi yoyote yanayoendelea hapa tunajiuliza ni nini kitafanyika ebu, jiulize leo ni tarehe tatu lakini hakuna jambo lolote linaloendelea”alisema Thadei,” amesema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Athumani Masasi, alitopatafutwa kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia suala hilo alijibu kuwa hayuko tayari kujibu masuala hayo wala kutoa majibu kwa sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment