Al-Shabab yatia doa uchaguzi Kenya

Askari wa Al-Shabab


ZIKIWA zimebaki siku tano kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini Kenya, hali ya usalama imeendelea kuwapa wasiwasi wananchi kufuatia mashambulizi pembezoni mwa pwani ya nchi hiyo, anaandika Catherine Kayombo.
Mashambulizi hayo yamefanyika maeneo ya Lamu, Mandera na maeneo ya jimbo la Lafey na wa watu wanaohisiwa kuwa Al-Shabab. Watu hao wamefanya mashambulizi ya mfululizo kwa siku mbili jumatano na Alhamis wakisababisha vifo vya watu takriban wanane.
Washambuliaji hao walivamia basi la abiria jana katika eneo la Lamu na kujeruhi watu watano. Pia Alhamis walivamia offisi za polisi katika Jimbo la Lafey na kuua polisi huku wengine wakijeruhiwa.
Kufuatia mashambulizi hayo, wakazi wa Pwani wamepata wasiwasi juu ya usalama wao kuelekea uchaguzi, kupelekea wengine kukimbia makazi yao. Wametoa rai kwa serikali kutozembea katika ulinzi hasa katika maeneo yanayoonekana kuwa hatarishi na yenye historia ya kuvamiwa na waasi.
Aidha, katibu katika wizara ya usalama joseph Bonieth amewahahakikishia wakazi wa Lamu na Mandera kuwa serikali itahakikisha ulinzi unakuwepo, na watu wasihame wala kukimbia maeneo yao kuhofia uvamizi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment