araza la Taifa la Mitihani (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2017.
Kwa mwaka 2017, baraza hilo limedaiwa ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 2.4 kutoka mwaka 2016, idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani ni 909,950 na wanafunzi 662,035 wamefaulu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo, Ijumaa, Mkoa wa Dar es Salaam umeibuka kidedea kitaifa ukifuatiwa na Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza na Katavi.
Ubora wa mkoa wa Dar es salaam unatokana na kati ya wavulana kumi bora kitaifa, watano wanatoka shule za mkoani humu, wanne wakitoka mkoani Kagera na mmoja Geita.
Na katika shule kumi bora kitaifa, Kagera imefanikiwa kutoa shule nne huku katika shule kumi zilizofanya vibaya zaidi, shule sita zinatoka katika mikoa ya Singida na Tanga kila mmoja ukitoa shule tatu (3).
Kwa upande wa shule bora za wasichana kumi bora kitaifa, wasichana sita wanatoka shule moja ambayo ni Sir John ya Tanga huku Kati ya watahiniwa kumi bora kitaifa, sita ni wavulana na wanne ni wasichana wakiongozwa na Hadija Ally na Naseem Said.