Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Aron Mbogho awakamata na kuwaweka ndani watendaji watatu wa kituo cha afya cha Kisangara baada ya kuwachangisha wananchi fedha za mafuta ya gari la kubebea wagonjwa.
Utaratibu huo ulikatazwa na serikali hatua ambayo pia inadaiwa kusababisha mgonjwa kufariki akiwa ndani ya gari hilo wakati linasubiri fedha za mafuta.
Akizungumza na ITV, Mbogho amesema kitendo kilichofanywa na watendaji hao hakikubaliki na ni cha makusudi kwani hata kama kulikuwa na tatizo la mafuta ziko njia nyingine ambazo zingeweza kutumika kuwafikisha wagonjwa kwenye tiba na hawakutaka kuutumia.
Wakisimulia mkasa huo baadhi ya ndugu wa mgonjwa aliyepoteza maisha wamesema siku ya tarehe 5/10/2017, katika eneo la Kisangara vijana watatu waliokuwa kwenye pikipiki waligongwa na gari majira ya saa 12 jioni na walipofikishwa kwenye kituo cha afya waliandikiwa kwenda KCMC na ndipo wakatakiwa kutoa 50,000 kwa ajili ya mafuta.
Wamesema pamoja na majeruhi hao kuingizwa kwenye gari la wagonjwa walianza kuzunguka mitaani kuchanga
hadi saa tatu usiku wakipopazipata na wakiwa njiani kwenda KCMC mmoja alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu
hadi saa tatu usiku wakipopazipata na wakiwa njiani kwenda KCMC mmoja alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu
0 comments :
Post a Comment