Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zakaria Hanspoppe amesema ana imani na mwenyekiti mpya wa Bodi ya ligi, Clement Sanga, licha ya kuwa anatoka kwa mahasimu wao katika soka la Bongo, Yanga SC.
Hanspoppe amesema anamfahamu vizuri Sanga na anaukubali utendaji wake wa kazi huku akimtaja kuwa mtu mtulivu na asiyekuwa na makuu.
Pamoja na kuonesha kukubali uwezo wake, kiongozi huyo wa Simba amempa angalizo kwa kumtaka kusimamia haki na kutokubali bodi hiyo kuyumbishwa kwa misingi ya itikadi za Yanga na Simba hasa wakati wa kufanya maamuzi mbalimbali.
“Pamoja na kwamba ni kiongozi wa Yanga, aendelee na uyanga wake lakini atende haki,” amesema Hanspoppe.
Hanspoppe pia amemtaka Sanga na uongozi mzima wa bodi hiyo uliochaguliwa Oktoba 15, mwaka huu kuifanya bodi hiyo kuwa huru, na kutorudia makosa ya uongozi uliopita wa kukubali kuingiliwa na TFF katika uamuzi wa kuipa Simba pointi tatu za Kagera Sugar.
Jambo jingine alilotaka Sanga alifanyie kazi ni suala la ratiba ya ligi, akitaka kutopanguliwa mara kwa mara kwa ratiba hiyo kama ilivyokuwa misimu
0 comments :
Post a Comment