Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ambapo baadhi ya mawaziri wamepoteza nyadhifa zao, wengine wakipandishwa nafasi na wengine wapya kuongezwa.
Rais amefanya mabadiliko pia katika wizara mbili ambapo wizara hizo zimegawanywa, jambo lililofanya wizara kuongezeka kufikia 21 kutoka 19 zilizokuwapo.
Wizara zilizogawnywa ni Wizara ya Nishati na Madini ambayo imekuwa wizara mbili zinazojitegemea, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini pamoja na Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambayo imegawanywa kuwa Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mbali na mawaziri na manaibu wao, Rais Dkt Magufuli ametangaza kuteua Katibu Mkuu mpya wa Bunge. Hapa chini ni orodha ya Mawaziri, Manaibu Waziri wapya walioteuliwa. Baadhi yao ni wapya katika baraza,
huku wengine wakipandishwa kutika manaibu kuwa mawaziri, na wachache wakihamishwa wizara.
1. Waziri wa Nchi, O×si ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora- George Huruma
Mkuchika
Mkuchika
2. Waziri wa Nchi, O×si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)- Selemani Said Jafo
3. Naibu Waziri wa Wizara Muungano na Mazingira- Kangi Alphaxard Lugola
4. Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa
5. Waziri wa Kilimo – John Tizeba
6. Naibu Waziri wa Kilimo- Mary Chuki Mwanjelwa
7. Waziri wa Mifugo na Uvuvi- Luhaga Mpina
8. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi- Abdallah Ulega
9. Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano- Elias John Kwandikwa
10. Waziri wa Nishati- Merdadi Kalemani
11. Naibu Waziri wa Nishati- Subira Khamis Mgalu
12. Waziri wa Maliasili na Utalii- Khamis Kigwangalla
13. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii- Japhet Ngailonga Hasunga
14. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji- Mhandisi Stella Manyanya
15. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia akitokea Wizara ya Mifugo- William Ole Nasha
16. Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Juliana Daniel Shonza
17. Katibu wa Bunge -Stephen Kagaigai. Aliyekuwepo, Dkt. Thomas Kashi Kashililah atapangiwa kazi nyingine
0 comments :
Post a Comment