Mkemia Mkuu wa serikali Profesa Samuel Manyele ametoa sababu inayowafanya kupima mkojo wa watu wanaotuhumiwa uhalifu mbali mbali, jambo ambalo liliibua mzozo mkubwa lilipotakiwa kufanyika kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Prof. Manyele amesema mpelelezi ana haki ya kutaka kitu ambacho kitamuongoza kwenye upelelezi wake, hivyo yeye kama mkemia mkuu huhitaji mkojo kwa kuwa mkojo ndio husafisha mwili, na ndio sampuli pekee ambayo utaipata kwa muhusika bila kutoboa mwili wake, ili kugundua iwapo mtuhumiwa amefanya kosa kutokana na matatizo ya akili.
“Wapelelezi wana haki ya kuchukua kielezo chochote, kama mtu amefanya kosa kwa kutumia kitu ambacho kinaharibu akili mfano dawa za kulevya, bangi au mirungi, maana yake ni kwamba uthibitisho wake utapatikana kutoka mwilini mwake, na sampuli ambayo mkemia mkuu anaitumia ambayo haihusiani na kutoboa mwili wa mtu ni mkojo, mkojo ndio unasafisha mwili, kemikali zote tata zinapita kwenye mkojo, kwa hiyo sisi tukiipata tunachunguza kuna nini, lengo hasa ni kuangalia matumizi ya vitu ambavyo huenda vinampelekea kufanya uhalifu”, amesema Prof Manyele.
Hivi karibuni kumekuwa na mzaha unaofanyika kwa wananchi kwa kuitisha kipimo cha mkojo, baada ya baadhi ya watu wanaotuhumiwa kufanya uhalifu akiwemo Tundu Lissu, muigizaji Wema Sepetu, Mfanya biashara Yusuph Manji kutakiwa